Mwanamuziki wa Kenya Bien Baraza amenyakua tuzo ya Msanii Bora Afrika Mashariki katika tuzo za kifahari za Trace Awards 2025 zilizoandaliwa kisiwani Zanzibar.
Mwimbaji huyo wa Sauti Sol aliibuka mshindi katika kitengo chenye ushindani mkubwa, akiimarisha nafasi yake miongoni mwa nyota bora wa muziki Afrika Mashariki.
Bien ameyaangusha baadhi ya majina makubwa katika muziki wa Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na Diamond Platnumz wa Tanzania, Zuchu, Marioo, na Harmonize, Joshua Baraka wa Uganda na Rophnan wa Ethiopia.
Bien Kama mteule pekee wa Kenya katika kitengo hicho, ushindi wake umekuwa mkubwa na wa kujivunia kwa nchi na wafwasi wanaofuatilia mziki wake.
Kabla ya kupokea tuzo hiyo ya kutamini, Bien alitoa onyesho la kuvutia, akiwapamba watazamaji na sauti yake ya kipekee na kutambulisha uwepo kwenye jukwaa. Utendaji wake ulikuwa moja ya mambo muhimu ya usiku, huku akionesha kwamba bado ana nguvu katika tasnia ya mziki.
Ushindi wa Bien haujaimarisha tu nafasi yake binafsi bali pia unaangazia ushawishi unaoongezeka wa muziki wa Kenya katika jukwaa la Afrika. Kwa ushindi huu, nyota huyo wa Sauti Sol anaendelea kuhamasisha kizazi kipya cha wasanii huku akikuza muziki wa Kenya kwa urefu zaidi.
Msanii wa Tanzania Harmonize alimpa zawadi ya mkufu mwanamziki huyo wa kenya Bien ikiwa ni ishara ya heshima na kupongezwa.
Bien ni msani ambaye anahusishwa na Bendi ya Sauti Sol ambayo inawashirikisha, Bien-Aime Baraza mwenyewe, Wills Chimano, Savara Mudigi, Polycarp Otieno, Phelomena Nyangweso na Myles Olet.
Tuzo za Trace Awards huhusisha muziki wa Kiafrika katika aina mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Afrobeat, Bongo Flava, Genge, Amapiano, na kadhalika.
Sherehe za mwaka 2025, zimefanyika jijini Zanzibar nchini Tanzania zikiwaleta wanamziki kutoka mataifa mbali mbali kutoka africa na inje ya Afrika.